Inawezekana ulikuwa na maswali mengi kuhusu shughuli za viwanda nchini kikiwemo kile cha Tanganyika Packers sasa basi leo tumempata majibu kwa Katibu mkuu wa wizara ya Viwanda na Bishara, Uledi Mussa.
Katibu huyo akizungumza na ripota wa millardayo alisema..’Jana
nilikuwa na kikao na katibu mkuu kiongozi sasa tunataka kujenga
viwanda vya nyama vikubwa vya kisasa kimoja kitajengwa Dodoma, kingine
kitajengwa Kibaha, kingine kitajengwa Mbeya hivyo viwanda vitakuwa vya
utaalamu wa hali ya juu kwa hiyo pale Tanganyika Packers huwezi kuweka
huduma ya machinjio ya nyama pale kwani tuna mpango wa kufanya kitu
kingine pale‘ – Uledi Mussa
‘Kwa hiyo
kwa maana ya sekta sasa ina maana saa hivi tunazungumzia viwanda kwa
sekta zote kwa upande wa mifungo tunasema tutakuwa na viwanda vya kisasa
vya nyama, kwa upande wa Samaki hivyo hivyo na kwa upande wa misitu
lazima tuache kuuza magogo tuanze kuuza
mbao tuuze furniture ambazo ni za kisasa sasa maana yake huo mpango wa
miaka mitano ujao ambao utatilia maanani viwanda ni lazima tutawekeza
nguvu zote tutajichimbia kwenye viwanda tuone tunaibukaje‘- Uledi Mussa

Note: Only a member of this blog may post a comment.