Thursday, September 10, 2015

Anonymous

HABARI MBAYA Kwa Mashabiki wa MAN UTD Kuhusu Louis Van Gaal na Wachezaji wa Timu Hiyo!


Kocha wa Manchester United Louis van Gaal alijiunga na klabu ya Man United toka mwaka 2014 akichukua mikoba ya David Moyes aliyetimuliwa kazi. Imeripotiwa kuwa Van Gaal sio kocha rafiki na wachezaji, kitu kilichopelekea kumkosa Pedro Rodriguez.
Van-Gaal_2989166b
September 10 stori iliyofichuka ni kuwa Louis van Gaal aligombana na wachezaji toka msimu wa Ligi Kuu haujaanza, stori kutoka  mtandao mirror.co.uk unaeleza kuwa kikubwa kilichopelekea Van Gaal kupishana na wachezaji wake, ni aina ya mfumo anaotumia kuwasliliana na wachezaji sio rafiki, hivyo kujikuta akigombana na wachezaji kutokana na ukali wake.
Stori inasema kuwa wakati timu ipo Marekani kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya, Van Gaal aliwakataza wachezaji kutembea, wala kufanya kitu chochote kwa madai kuwa kilichowapeleka ni maandalizi ya msimu na sio kingine chochote. Hivyo wachezaji wakawa na ratiba ya kula, kufanya mazoezi na kulala.
hi-res-7edef97d187192b0a9cef8abd89aac64_crop_north
 Kocha Louis van Gaal sio rafiki wa wachezaji inadaiwa mastaa wengi wa klabu hiyo wamewahi kutofautiana na kocha huyo. Wachambuzi wa masuala ya soka wanasema kwa ushirikiano huu ni ngumu kupata mafanikio akiwa na wachezaji ambao hana mahusiano nao mazuri. Di Maria amewahi kukiri moja kati ya sababu zilizomfanya ahame Man United ni Van Gaal.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.