Sunday, September 20, 2015

Anonymous

Jb Avutia Nyumbani, Aeleza Kukatishwa Tamaa!


Muigizaji na muongozaji mkongwe wa filamu hapa Bongo, Jacob Stephen amewataka mashabiki kupenda kazi za nyumbani ili kuzipa uzito kwenye nchi za jirani.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa filamu mpya ya MAHABUSU ambayo kwasaa ipo madukani; ambayo imemshirikisha marehemu Kuambiana, JB alisema kuna tabia ya wapenzi wa Bongo Movies kuponda kazi za wasanii kwa madai kuwa hazina uhalisia.

Hali hiyo alisema JB inafanya soko la kazi za wasanii kuwa ngumu pia katika nchi jirani.
"Hakuna kitu kigumu kama kuandaa na kutengeneza filamu mpaka ikamilike lakini baadhi ya mashabiki wanatukatisha tamaa na ndiyo chanzo cha wasanii wengi kuishia njiani," alisema JB.
Chanzo: Lete Raha

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.