Sunday, September 20, 2015

Anonymous

MAREKANI YAWAKA MOTO, NYUMBA 1000 ZATEKETEA CALIFORNIA

Nyumba 1000 zimeteketea California
Nyumba 1000 zimeharibiwa na moto ambao umekuwa ukiwaka kwa zaidi ya wiki moja California nchini Marekani.
Maafisa wa idara ya usalama wa umma Kaskazini mwa jimbo la California nchini Marekani wanasema kuwa moto huo huenda ukaenea zaidi na kusababisha uharibu mkubwa zaidi.
Takriban watu 5 wameaga dunia kutokana na moto huo. Takriban watu 5 wameaga dunia kutokana na moto huo
Idara ya kupambana na majanga imeonya kuwa moto huo umesambaa katika eneo kubwa lenye mamia ya kilomita mraba na huenda watu wengi zaidi wakalazimika kuhama makwao.
Maafisa wanasema kuwa moto wa kipindi hiki katika jimbo la California ambao mara nyingi hutokea kati ya mwezi Septemba na Oktoba unatarajiwa kuwa mkubwa zaidi katika historia.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.