Habari njema kwa watumiaji wa mtandao wa kushare picha wa Instagram
ni kuwa, huduma ya ‘Instagram Direct’ sasa imeboreshwa zaidi.
Instagram Direct ni huduma inayowawezesha watumiaji kuweza kutumiana
picha, video na ujumbe binafsi kwa mtu mmoja, au kundi la watu
atakaowachagua mwenyewe bila mtu mwingine kuona.
Hivi sasa kuna ki mshale kimeongezwa pembeni mwa icon ya like na
comment chini ya kila post. Kazi yake ni pale utakapoipenda picha au
post ya mtu unaweza kumtumia mtu kwa kukibonyeza kimshale hicho kwa
kutumia Instagram direct.
Pia hivi sasa uwanja wa kuchat wa Instagram direct umepata muonekano unaofanana kama wa Messenger.
Katika maboresho hayo pia sasa hakuna ulazima wa kumtumia picha mtu
ili uweze kuanza kuchat nae kwa ujumbe, ukiwa kwenye uwanja wa Instagram
direct, unaweza kuchagua ‘send message’, kasha unachagua jina la
unayetaka kumtumia kwa kusearch jina lake na kuanza kumuandikia ujumbe
moja kwa moja bila picha.
Ili kuyaona mabadiliko hayo mtumiaji anatakiwa ku update app ya Instagram kwenye simu yake.

Note: Only a member of this blog may post a comment.