Stori kubwa kutoka Las Vegas Marekani September 09 2015 ilikuwa ishu ya Ndege ya British Airways kuanza kuwaka moto katika Uwanja wa Ndege wakati ikiwa na abiria 159 ndani pamoja na wahudumu 13.
Ndege ilikuwa tayari imeanza safari kwenye njia ya kurukia lakini injini ya kushoto ikawaka moto, Rubani Chris Henkey ndiye
aliyetoa taarifa ya kuomba msaada wa dharura huku akiendelea na
jitihada za kutafuta njia ya kusimamisha ndege ili kuokoa abiria waliomo
ndani ya Ndege.
Baada ya ajali hiyo, Rubani wa ndege
hiyo ametangaza kwamba kwa sasa inatosha na anaona itakuwa sawa kama
akistaafu >>> ‘Najua Magazeti
yataniandika kunisifu kwa ushujaa lakini kulikuwa na Marubani watatu
ndani ya ile ndege ambao wana mchango wao pia’- Chris Henkey.
Henkey
alitoa taarifa ya Ndege kuwa na dharura wakati tayari Ndege iko kwenye
njia ya kurukia lakini sekunde 40 mbele akaomba msaada wa Vikosi vya
Zimamoto baada ya moto huo kuanza huku Ndege ikiwa bado inatembea kwenye
njia ya kurukia.
Abiria 14 walitoka na majeraha madogo
madogo ambayo walipata katika harakati za kujiokoa lakini hakuna abiria
hata mmoja aliyefariki au kupata tatizo kubwa.
Hiki ni kipande cha Video kilichorekodiwa na walioshuhudia ndege hiyo ikiwaka moto.

Note: Only a member of this blog may post a comment.