Mzazi ana nafasi kubwa ya kuitengeneza njia ya maisha ya mwanaye iwe
ya lami au ya mashimo ya kutosha, kwasababu mengi wayafanyayo watu
wazima wa sasa yalichangiwa na makuzi ya udogoni.
Wiz Khalifa na mama yake
Mama mzazi wa rapper Wiz Khalifa wa Marekani, Katie ‘Peachie’
Wimbush-Polk amekiri kuwa yeye ndiye aliyemfundisha staa huyo kutumia
kilevi cha bangi toka akiwa mdogo.
Akizungumza na The Sun, Peachie alisema kuwa kabla hajaenda kwenye
shughuli zake na kabla Wiz hajaenda shule enzi za udogo wake walikuwa
wakivuta bangi pamoja, na kuongeza kuwa alipata tabia hiyo kutoka kwake.
“Before I went to work, before he went to school, it was our way
of bonding. We would smoke together. He got his habit from his mother.”-
Peachie
Note: Only a member of this blog may post a comment.