Emmanuel Adebayor ameachwa kwenye kikosi cha Tottenham Hotspur chenye wachezaji 25 kwaajili ya Premier League.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 alitarajiwa kuondoka White Hart
Lane lakini hakuna klabu iliyofikia makubaliano ya gharama za
kumchukua.
Kutokana na hilo mchezaji huyo wa Togo ataendelea kupiga benchi Spurs
hadi January pale ambapo atakuwa akifanya mazoezi na wachezaji wa ziada
na timu ya vijana.
West Ham waliaminika kuwa mbioni kumsainisha kwa mkopo lakini walikuwa wameshafikia kikomo cha kuchukua wachezaji wa mkopo.
Hata hivyo mashabiki wengi wa Spurs wamekosoa uamuzi huo wakiamini
kuwa ni bora angewekwa kwenye kikosi hicho hata kama angekuwa mchezaji
wa ziada.

Note: Only a member of this blog may post a comment.