Linah anadai tayari ameshatambulishwa kwa wazazi wa mpenzi wake mpya ambaye ni raia wa Uganda, Williams Bugeme.
Hata hivyo Linah ameiambia Bongo5 kuwa sasa hivi wameamua kupunguza kujionyesha sana ili wapate muda wa kufanya kazi.
“Namshukuru Mungu mama mkwe alinipokea vizuri sana,” Linah
ametuambia. “Wadogo zake pamoja na marafiki. Najivunia kuwa naye sema
sasa hivi tumeamua tupunguze kujionyesha. Kama mapenzi yapo tu huu ni
wakati wa kufanya kazi kwanza,” ameongeza.
Kwa upande mwingine Linah ambaye ni miongoni mwa wasanii waliotajwa
kuwania tuzo za kimataifa za Afrima, amewataka watanzania kuunga mkono
kazi zake pamoja na kumpigia kura.
-via bongo5

Note: Only a member of this blog may post a comment.