Saturday, September 12, 2015

Anonymous

22 PICHAZ: Mnyama Aunguruma Tanga...Shuhudia SIMBA SC Walivyoitafuna African Sports Leo!

September 12 ndio siku ambayo pazia la Ligi Kuu Tanzania bara limefunguliwa kwa michezo kadhaa kupigwa katika viwanja tofauti tofauti, mchezo uliyokuwa umeteka hisia za watu wengi ni mechi kati ya African Sports dhidi ya Simba mechi iliyochezwa katika uwanja wa Mkwakwani Tanga.
Mvuto wa hii mechi unatokana na rekodi ya klabu ya Simba kwa hivi karibuni kutofanya vizuri katika mechi zake za Ligi Kuu alizocheza Tanga katika uwanja wa Mkwakwani. Huku kwa upande wa African Sports ndio wamerudi Ligi Kuu baada ya kushuka miaka kadhaa nyuma hivyo hawakuwa tayari kupoteza mechi yake ya kwanza ya msimu, tena katika uwanja wake wa nyumbani.
DSC_0161
Wachezaji wa African Sports wakimsukuma Mgosi baada ya kumfanyia faulo mchezaji mwenzao
Mechi imemalizika kwa klabu ya Simba kuondoka na ushindi wa goli 1-0 goli pekee lilifungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda aliyewahi kuichezea Yanga Hamisi Kiiza, kipindi cha pili. Licha ya kukosa nafasi kadhaa Simba ilifanikiwa kutumia nafasi moja kutoka kwa nahodha wao Musa Mgosi na Kiiza kutia nyavu kwa kichwa.
DSC_0065
Ayoub Masoud akijaribu kumpita Peter Mwalyanza wa Simba
DSC_0067
Ayoub Masoud akiwania mpira na Peter Mwalyanza
DSC_0198
Benchi la klabu ya African Sports
DSC_0176
Hassa Kessy wa Simba akichuana na Rahm Abdallah
DSC_0197
Kocha wa African Sports Joseph Lazaro
DSC_0189
Simon Serunkuma akiingia kuchukua nafasi ya Mwinyi Kazimoto
DSC_0186
Kocha wa Simba Dylan Kerr akitoa maelekezo
DSC_0182
Rahm Abdallah akimtoka mchezaji wa Simba
DSC_0158
Nahodha wa Simba Musa Mgosi akipiga krosi
DSC_0173
DSC_0138
Musa Mgosi akipata huduma ya kwanza baada ya kupata maumivu
DSC_0135
Hamisi Kiiza akisali baada ya kufunga goli
DSC_0140
Mgosi akitoka nje baada ya kupata maumivi
DSC_0143
Musa Hassan Mgosi
DSC_0134
Wachezaji wa Simba wakishangilia goli huku mshika kibendera akiwarudisha uwanjani
DSC_0132
DSC_0087
Mzozo wa wachezaji baada ya kufanyiwa faulo mchezaji wa African Sports
DSC_0086
DSC_0074
DSC_0055
Golikipa wa African Sports Yusuph Yusuph akiokoa goli

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.