Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo sasa
ni baba mkwe wa muimbaji wa ‘Shaghala Bhaghala’, Meninah Atick
aliyefunga ndoa na mwanae, Abdukarim Haule.
Kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania mahaba ya mtoto huyo wa Waziri
Muhongo, Peter Haule yamemfanya abadili dini na kuwa Abdulkarim Haule
ili aweze kumuoa Meninah ambaye ni muislamu. Wawili hao walifunga ndoa
huko Kigamboni wikiendi iliyopita.
Japo hajasema chochote kuhusu ndoa yake zaidi ya picha zinazoashiria ndoa yao, Meninah ameandika kwenye Instagram:
Usichague msichana ambaye ni mzuri duniani, chagua anayekupa
furaha duniani, maisha ni mafupi na huwezi jua kesho kuna nini, fanya
mazuri, asante Mungu kwa kila njia ninayopitia, nazidi kukumbuka kwa
kubadilisha maisha yangu na kutumaini milele

Note: Only a member of this blog may post a comment.