Mvuko alikuwa akiripoti kuhusu ziara ya rais wa Edgar Lungu aliyekuwa kwenye hospitali hiyo kutibiwa Malaria.
Video hiyo inamuonesha Mvuko na mtu wake wa kamera akizingirwa na vijana watatu ambao mwanzoni wanaonekana kama wapita njia lakini walisimama mbele na nyuma ya ripota huyo wakitaka wapewe simu na fedha. Vibaka hao walichukua vitu kadhaa vya Mvuko huku pia wakimfuata camera woman aliyekuwa hapo. Mwishoni mwa video hiyo, Mvuko anasikika akisema: We are being mugged.”


Note: Only a member of this blog may post a comment.