Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetangaza
kiama kwa watumiaji vibaya na wahalifu wote wa mitandao nchini, kuwa
siku zao zinahesabika kwani ifikapo Septemba mosi, mwaka huu, Sheria ya
Uhalifu wa Mitandao itaanza kutumika na wengi huenda wakaishia gerezani.
Mamlaka hiyo imebainisha kuwa kwa sasa Tanzania inaongoza kwa kuwa na watumiaji vibaya wengi wa mitandao ya kijamii, jambo linalosababisha taarifa za mitandao mingi kutoaminika hadi nchi za nje kutokana na kujaa uzushi, uongo, uchochezi na lugha na picha za matusi.
Meneja Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungy alikiri kuwa pamoja na kwamba mamlaka hiyo imefanya kazi kubwa ya kuelimisha jamii juu ya utumiaji sahihi wa mitandao hiyo, bado matumizi yake si mazuri hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi na kwa watu maarufu.
“Napenda kuwatahadharisha Watanzania na watumiaji wa mitandao hii kwa ujumla kuwa sheria hii si ya kupuuzwa, kwani kwa hali ilivyo wengi watatozwa faini na watashindwa kulipa na kuishia gerezani,” alisisitiza.
Alisema kutokana na kukithiri kwa matumizi mabaya ya mitandao nchini, kwa sasa nchi nyingi haziamini tena taarifa za mitandao ya kijamii na wala hawazitumii hali inayopaswa kubadilishwa.
“TCRA tumebaini kuwa watu wengi wanatumia mitandao hii lakini hawajui hasa matumizi yake sahihi, tunashauri kabla mtu hajafungua mtandao wake kama vile blogu, ukurasa wa facebook au hata whatsApp lazima wajielimishe kwanza kuwa wanafungua kwa malengo gani, na wataitumiaji kwa manufaa yao na si vinginevyo,” Mungy.
Alisema mamlaka hiyo kazi yake kubwa ni kusimamia matumizi ya mitandao hivyo kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola, itahakikisha inadhibiti kwa kuelimisha na kuwabaini wale wote wanaotumia vibaya mitandao hiyo.
“Kazi yetu sisi si kuwakamata hawa wahalifu, sisi tunasimamia na tuna uwezo wa kuwatambua wale wote wanaotumia vibaya mitandao hii hata kama watabadilisha kadi zao za simu mara 300 na kubadili majina, tuna uwezo wa kuwatambua na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria pale tunapotakiwa kwa mujibu wa taratibu,” alisisitiza
Alisema tayari wameshaanza kampeni ya kuelimisha matumizi sahihi ya mitandao kupitia vipindi na semina zinazojumuisha kada mbalimbali muhimu kama vile wasanii na vyombo vya habari juu ya kujihadhari na matumizi mabaya ya mitandao.
“Hivi karibuni tulifanya semina ya wasanii ambao ndio waathirika wakubwa wa matumizi haya ya mitandao na kuwaelimisha namna ya kuitumia mitandao hii, pia vyombo vya habari tumevielimisha na kuvisisitiza kutotegemea taarifa za mitandao hasa kipindi hiki cha uchaguzi kwa kuwa nyingi si sahihi,” alisema bosi huyo wa TCRA.
Tayari Rais Jakaya Kikwete ameshasaini Sheria hiyo ya Makosa ya Mtandao ya Mwaka 2015 na inatarajiwa kuanza kufanya kazi rasmi Septemba mosi, mwaka huu. Sheria hiyo katika eneo la adhabu kwa wahalifu wa mtandao pamoja na wasambazaji wa picha za utupu na ngono, wasambazaji wa taarifa za uongo, za kibaguzi na matusi na watu wengine wanaofanya udanganyifu unaohusu kompyuta, adhabu ni kwenda jela hadi miaka 10 au kulipa faini isiyopungua Sh milioni 50.

Note: Only a member of this blog may post a comment.