Wakizungumza na ITV katika kata ya Lukozi iliyopo jimbo la Mlalo wilayani Lushoto wakazi hao wamesema wabunge waliochaguliwa katika vipindi vilivyopita wamekuwa wakitoa ahadi nyingi bila ya utekelezaji wowote hivyo wametoa masharti kuwa mbunge ajaye lazima aanze kutatua kero za ukosefu wa kituo cha afya,uchakavu wa barabara na shule za sekondari kuwa mbali ili kuwapunguzia adha wananchi.
Kwa upande wao baadhi ya wagombea kati ya 15 waliojitokeza kuomba ridhaa ya wananchi kuchaguliwa kuwawakilisha wananchi Bungeni wakijibu masharti hayo baadhi yao wameeendelea kutoa ahadi ikiwa ni pamoja na kukabiliana na changamoto mbali mbali ikiwemo ukosefu wa huduma za afya,uchakavu wa barabara pamoja na masoko ya mazao ya mboga mboga ambayo ndio zao kuu la wakazi wa wilaya ya Lushoto.

Note: Only a member of this blog may post a comment.