Mkazi wa Kitongoji cha Kitukila , Kilombero Mkoni Morogoro Clemence Ligoma amenusurika kufa baada ya kutafunwa na fisi wakati akiwa usingizini kwenye makazi yasiyo rasmi.
Ligoma alikutwa na dhahama hiyo akiwa amelala nje usiku wa manane.
Inaelezwa kuwa fisi huyo alipita eneo
hilo na kumtafuna mguu hadi kubakia mfupa ndipo alipozinduka kutoka
usingizini na kaunza kuomba msaada.
Shuhuda wa tukio hilo Ibrahimu Muhamed alisema mzee huyo alipata jeraha kubwa katika mguu wake na kukimbizwa katika kituo cha afya kwa matibabu zaidi.
Alisema jitihada za kumsaka fisi huyo
zinafanyika ili asiendelee kulata madhara kwa wananchi na kuwataka watu
kuacha kukaa katikamazingira hatarishi kwa maisha yao.


Note: Only a member of this blog may post a comment.