Deogratius Mongela na Chande AbdallahI
INAUMA sana! Katika hali isiyo ya kawaida, mkazi wa Kata ya Mwembe Mkavu, Wilaya ya Bagamoyo, Pwani, Ramadhani Mloli (37) amemuua mkewe, maarufu kwa jina la Mama wa Naironi kwa kumchoma visu sehemu mbalimbali za mwili kisha na yeye kujiua kwa kisu pia.
INAUMA sana! Katika hali isiyo ya kawaida, mkazi wa Kata ya Mwembe Mkavu, Wilaya ya Bagamoyo, Pwani, Ramadhani Mloli (37) amemuua mkewe, maarufu kwa jina la Mama wa Naironi kwa kumchoma visu sehemu mbalimbali za mwili kisha na yeye kujiua kwa kisu pia.
Tukio hilo la kikatili lilijiri Agosti 21, mwaka huu, saa moja na
nusu asubuhi nje ya Ofisi ya Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata),
iliyopo Bagamoyo.Kwa mujibu wa chanzo, Ramadhani na mkewe huyo
walitengana kufuatia ugomvi usiojulikana ambapo mke huyo alikwenda
kuishi kwa ndugu zake, Kibaha, Pwani huku akiwa amefungua kesi Bakwata
akidai talaka.
Chanzo kikasema kuwa, siku ya tukio, mwanamke huyo alifika kwenye ofisi hizo mapema kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo.Chanzo kinasema kesi hiyo ilitakiwa kusikilizwa saa tatu asubuhi, lakini ilikatishwa na tukio hilo baada ya Ramadhani kuwahi eneo hilo na kutoa kisu alichokificha na kumchoma nacho marehemu sehemu mbalimbali za mwili mpaka kukata roho.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, baada ya kutekeleza mauaji
hayo, Ramadhani naye alijichoma kisu huku akijikata bila huruma eneo
zima la tumbo na kuutoa utumbo nje kisha akachukua mchanga na kujipakaza
kwenye utumbo kabla ya kuishiwa nguvu na kudondoka chini akiwa hoi.
“Ilikuwa inatisha sana! Halijawahi kutokea tukio la aina hii hapa
Bagamoyo. Haraka sana tuliwachukua na kuwakimbiza Hospitali ya Wilaya ya
Bagamoyo. Lakini wakati huo mwanamke hakuonesha dalili ya kuwa hai,”
alisema mmoja wa wasamaria wema waliojitokeza kuwapeleka hospitali.
Waandishi wetu walifika katika hospitali hiyo na kukutana na Mganga Mkuu Mfawidhi, Emmanuel Nhonoli aliyesema:
“Tuliwapokea wakiwa katika hali mbaya sana. Katika vipimo vya awali
iligundulika kuwa, mwanamke alishafariki dunia lakini mwanaume alikuwa
mahututi na baadaye aliaga dunia.”
“Mpaka sasa hakuna anayejua kiundani tatizo hasa zaidi ya wao
wenyewe. Ila siku moja kabla ya tukio, mwanaume alinunua kisu na kukinoa
sana akisema kesho katika hukumu yao kule Bakwata atafanya kitu cha
ajabu sana, hakuna atakayetegemea.
“Inaonekana Rama (Ramadhani) alikusudia kufanya mauaji haya maana
kaacha ujumbe unaosema mali zake zote warithi ni watoto wake wanne huku
akimtaja msimamizi mkuu kuwa ni kaka yake mkubwa aitwaye Twaha,” alisema
jirani mmoja.
Naye mjumbe wa shina katika eneo la Mwembe Mkavu, Kata ya Kidongo Chekundu, Mohamed Khamis alisema:
Mazishi ya marehemu hao yalifanyika Agosti 22, mwaka huu ambapo
Ramadhani alizikwa nyumbani kwake huku mwanamke akizikwa Kibaha kwa
ndugu zake.

Note: Only a member of this blog may post a comment.