Akiongea na waandishi wa habari mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoani simiyu,Adili Elinipenda amsema kuwa dereva huyo ambaye pia ni mratibu elimu kata ya nyangokolwa wilayani Bariadi, alikamatwa majira ya saa tano usiku katika kijiji cha nguliguli wilayani maswa akiwa anaendesha gari hilo ambalo baada ya kulikagua walikuta pesa kiasi cha shilingi laki nne zenye noti mpya za elfu mbilimbili.
Amesema kuwa baada ya maafisa hao kumhoji amekiri kuwa gari hilo lilikodiwa kugawa pesa hizo kwa wajumbe na mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Maswa Peter Bunyogori ambaye pi ni mgombe wa ubunge kwa tiketi ya chama cha mapinduzi.
Kufuatia hali hiyo mkuu huyo wa TAKUKURU ameonya wagombea wa vyama vyote vya siasa katika mkoa huo kuachana na vitendo vya rushwa ikiwa ni pamoja na kuwahonga wajumbe ,kuwakodia nyumba za kulala wageni na kuwapa zawadi za aina yeyote kwa ajili ya ushawishi na kwamba taasisi hiyo imejipanga vilivyo kwani haitamuonea huruma mgombea yeyote hata kama anatoka chama tawala CCM.

Note: Only a member of this blog may post a comment.