Friday, August 28, 2015

Anonymous

UKAWA Kwanini Mmekua Hivi?!

UKAWA kimya kimekuwa kingi kwanini siku zote munachelewa kuanza? uko ndani kuna nini simsikii Tundu Lissu, Mnyika wala chochote, kwenye media hatuwaoni ccm wameanza kampeni na sasa wameshaanza safari sehemu mbali mbali Television zote zinamuonyesha Makufuli kwanini?

Juzi tumemuona Lowassa tandale sasaiv baada ya marufuku hatuoni hatua nyengine yeyote, Mbowe kwanini huungani na Lowassa unafanya nini huko ndani ndani au kama hamkujiandaa tuambieni tupigie Kura Maruhaniii.

Leo nimeskia uwanja wa Jangwani hamjaruhusiwa ufunguzi wa kampeni ivi kwani ni lazima mfungue kampeni pale Jangwani?? kama Jangwani mumezuia huko mikoni na sehemu nyengine kwanini hamfanyi? kwanini hamfanyi kampeni viwanja vipo kibao kwanini siku zote mnakuwa wa mwisho muda wenyewe mfupi ccm wana take over mnatuumiza Matumbooo.

Hiyo team yenu ya Kampeni ipo wapiiii??? namuona Lowassa na Babu Juma Duni tu.!

Unaweza kuchelewa kumtangaza mgombea urais kwa kupata mtu Makini lakini sio kuchelewesha kuanza kampeni, UKAWA ni tumainio letu makamanda kwa nini kimyaa?

Mlisema Kampeni zikianza mwendo utakuwa mdundo mbona mmepwaya. Simuoni Halima Mdee na Bawacha yake wala chochote? Lema, Sugu mko kimya.
Kafulila tokea Imalize Escrow haongei chochote Lowassa anachafuliwa kwa ujinga kwanini hamtoi majibu??

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.