Thursday, August 20, 2015

Anonymous

SIMBA SC Kumleta Papa NIANG Kutoka SENEGAL? Hii ni Sababu Inayoongeza Uwezekano wa Kumpata!

tamuffjaro20090423_0268
Klabu ya soka ya Simba bado inaendeleza usajili wake kimya kimya kwani baada ya kusajili wachezaji kadhaa katika msimu huu bado huenda ikamuongeza mshambuliaji wa kimataifa wa Senegal aliyekuwa anaichezea klabu ya CF Mounana ya Gabon Papa Niang.
NIANG PAPA
Simba bado hawajathibitisha usajili huo kwani inaripotiwa atatua Dar Es Salaam ndani ya siku mbili hizi, uvumi wa mshambuliaji huyo kujIunga na Simba unatiwa nguvu kwa mchezaji huyo kuwa huru hadi hivi sasa hivyo huenda Simba ikatumia nafasi hiyo kumnasa.
tamuffjaro20090423_0268
Papa Niang aliyezaliwa December 5 1988 Matam Senegal amewahi kuchezea vilabu vya Vostok Oskemen ya Kazakhstan, Al-Shabab Sports Club ya Kuwait na kuichezea klabu ya CF Mounana ya Gabon aliyoichezea kwa takribani mwaka mmoja.
OT_236366
Licha ya dirisha la usajili kufungwa saa 6 usiku August 20 uwezekano wa Simba kumnasa staa huyo upo kwani baada ya kufungwa kwa dirisha la usajili usiku wa August 20 timu zinaruhusiwa kusajili ila kwa malipo ya Tsh 500,000/= kwa kila mchezaji itakao muongeza kikosini kabla ya msimu wa Ligi haujaanza.
CHANZO CHA HII STORI: SALEH JEMBE

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.