Baadhi ya wanachama wa CCM wakimkabidhi zawadi katika mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu.
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa tiketi ya CCM akihutubia jimbo la Hai.
Baadhi ya wanachama na wapenzi wa CCM wakiwa katika mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Arusha Mjini.
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa tiketi ya CCM akihutubia jimbo la Hai.
Baadhi ya wanachama na wapenzi wa CCM wakiwa katika mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Arusha Mjini.
Baadhi ya wanachama na wapenzi wa CCM wakiwa katika mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Arusha Mjini.
Burudani kwa wananchi na mgeni rasmi katika mkutano wa hadhara moshi Mjini.
Na Joachim Mushi, Arusha
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kikifanikiwa kushinda
Uchaguzi Mkuu wa Oktoba kitahakikisha mgambo wa halmashauri ya jiji
hawawasumbui kwa kamatakamata za wafanyabiashara ndogondogo ambao wengi
wao ni akinamama pamoja na vijana. Kauli hiyo imetolewa leo na mgombea
mwenza nafasi ya urais tiketi ya CCM, Bi. Samia Suluhu alipokuwa
akihutubia mkutano wa hadhara katika mkutano uliofanyika uwanja wa
Kilombero Jimbo la Arusha Mjini na kuhudhuriwa na umati wa wanaCCM na
wananchi wengine.
Akinadi ilani ya CCM alisema chama hicho kimeandaa utaratibu
mzuri wa fursa kwa akinamama na vijana wanaofanya biashara ndogondogo
hivyo itakuwa ni marufuku kwa mgambo wa jiji kukamata biashara za
akinamama na vijana wanaojitafutia ridhiki mjini. “…Iwapo CCM
itafanikiwa kuingia mjini naomba wale mgambo ambao uishi kwa kutegemea
kukamata kamata bidhaa za akinamama watafute kazi nyingine ya
kufanyanya…hatutaki mgambo wa kufanya kazi hizo ni marufuku,
” alisema mgombea huyo mwenza wa CCM, Samia Suluhu. Alisema
Ilani ya CCM imepanga kujenga viwanda vya kuchakata madini ili
kuhakikisha vijana wanapata ajira na kuweza kukuza vipato vyao, na
kufufua viwanda vilivyosimama kikiwemo cha ‘General Tyre’ ikiwa ni
mpango wa kumaliza tatizo la ajira kwa vijana. Aidha alisema mpango
mwingine ambao upo kwenye ilani ya CCM ni kushughulikia tatizo la
mikataba ya ajira ya madereva wa magari madogo na makubwa, “..
.Tukifanikiwa kuingia Ikulu kazi ya kwanza tutakayoipa Wizara ya
ajira ni kuhakikisha inafanya kazi ya kushughulikia mikataba ya ajira
kwa madereva wa magari madogo na makubwa,” alisema Bi. Suluhu. Aliongeza
Serikali ya CCM itaunda ufuko wa maji kuakikisha huduma za maji
zinakuwa za uhakika kwani Mkoa wa Arusha unashughuli nyingi na idadi ya
watu inakuwa kila uchao. Serikali ya CCM imepanga kushughulikia suala la
rushwa na vitendo vya ufisadi, uzembe ili kuhakikisha kasi ya maendeleo
inaongezeka. Awali kabla ya mkutano wa Arusha Bi. Suluhu alifanya
mikutano katika majimbo ya Hai, Siha na Arumeru yaliyopo mikoa ya
Kilimanjaro kabla ya kuingia Mkoani Arusha. Akiwa katika majimbo hayo
mgombea aliinadi ilani ya CCM pamoja na kuwanadi wagombea ubunge na
madiwani wa CCM wa maeneo hayo. Ambapo alisema Serikali ya CCM imepanga
kuboresha huduma za afya, elimu, uwezeshaji wa vijana na akinamama ikiwa
ni pamoja na kutenga shilingi milioni 50 kwa kila kijiji kwa ajili ya
kuwainua akinamama na vijana.

Note: Only a member of this blog may post a comment.