Mpenzi
msomaji wangu, leo nikupe siri kubwa ambayo huifahamu na huenda
unatafuta dawa ya kulienzi penzi lako au kulinogesha ili mpenzi wako
adumu na wewe.Nikueleze ukweli tu kwamba, hakuna dawa ya mapenzi katika
ulimwengu huu, dawa ni wewe mwenyewe hasa ukiamua kufuata misingi ya
mapenzi.
Inawezekana unajua ila unadharau au hujui kabisa sasa leo nitakuambia
dawa yenyewe ni nini.Hivi hujawahi kuona kitu ukikiangalia wewe
mwenyewe unakiona hakina maana au unakiona ni kidogo lakini ukamfanyia
mpenzi wako ndiyo unakuwa umemroga kabisa na kumfanya akuhitaji na
kutamani kuwa na wewe wakati wote?Miongoni mwa vitu ambavyo ni vidogo
lakini ni vikubwa kwa wapenzi wetu hasa wa kike ni pamoja na hivi
vifuatavyo.
Kumpikia
Mwanamke ukimpikia chakula kuanzia kukiandaa mpaka yeye akakila hii
huwa ni sumu kubwa ambayo humfanya ajione amefika. Siyo rahisi akaenda
kwa mwingine eti kwa kufuata pesa ama gari kwani mwanamke ni mtu wa
kuridhika kwa vitu vidogo wakati mwingine.Nakwambia mpenzi msomaji wangu
kwa sababu nimewasoma wanawake wengi wanapenda mwanaume anayejali na
mara nyingi kupikiwa huwa ni kitu adimu.
Wengi wetu tunajua hasa kwa mila za Kiafrika mwanamke ndiye
huwajibika jikoni kwa kumuandalia mwanaume, ni wachache ambao huamua
kumpikia mwanamke.Kutokana na uafrika wetu imefikia hatua ya watu
kumuona mwanaume anayempikia mwanamke kuwa amepewa limbwata kwa sababu
si kawaida, wanasahau kuwa kufanya hivyo ni kuongeza upendo kwa
mwanamke.
Hii ni dawa nyingine ambayo ukimfanyia mwanamke hujikuta anakumisi hata uwapo mbali.
Wanawake wengi ni wavivu wa kula au utakuta akila kidogo anaacha. Ili kuongeza mapenzi hebu jaribu kumlisha uone jinsi atakavyokula na wewe mpaka mwisho.Kitendo cha wewe kumlisha huwa kinamfanya ajihisi anapendwa sana kama mtoto na humpa nafasi ya kukudekea.

Utani
Watu wengi hujiuliza hivi f’lani alimpendea nini f’lani wakati hana
kitu. Siyo kitu kwa wakati mwingine nilichojifunza wanawake wengi
hupenda mwanaume ambaye anaweza kumfanya akacheka na kupoteza ‘stress’
alizonazo.
Mwanamke ukimpa nafasi ya kumtania au kumfanyia utani utakaoamsha kicheko huwa anakukumbuka wakati wote na kama ni mpenzi wake hutamani kuwa na wewe wakati wote.
Mwanamke ukimpa nafasi ya kumtania au kumfanyia utani utakaoamsha kicheko huwa anakukumbuka wakati wote na kama ni mpenzi wake hutamani kuwa na wewe wakati wote.
Vizawadi
Vizawadi vidogo vidogo kama pipi, apple, chokleti, keki siyo kwa
watoto tu hata watu wazima. Ukimpelekea mkeo zawadi kama hizo anathamini
na kuona umempa kitu kikubwa kuliko unavyodhani.
Wanawake hawatofautiani sana na watoto, nao hupenda kuoneshwa mapenzi kwa njia hii.
Kwa hivyo nilivyokuandikia hapo hakika ni vitu vidogo lakini ukimfanyia mkeo au mpenzi wako utaona jinsi penzi lenu litakavyochanua.

Note: Only a member of this blog may post a comment.