Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ .
Brighton Masalu
STAA wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kwa sasa
yupo ‘bize’ kwenye maombi kwa Mungu, kutokana na kile alichokiita,
kutumia muda mwingi kuwa katika ibada za kumcha Mungu.
Jumapili iliyopita, Lulu na mama yake, Lucresia Karugila walinaswa na
mwandishi wetu ndani ya Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar,
kulikokuwa na uzinduzi wa Albamu ya Tunapendwa na Mungu ya mwimbaji wa
nyimbo za Injili, Boniface Mwaitege.
Hata
hivyo, mwandishi wetu alipomuuliza Lulu kulikoni kuzama kwenye maombi,
alijibu kwa kifupi kuwa katika maisha ya duniani hakuna jipya, hivyo
yeye na familia yake wameona ni heri kumkabidhi Mungu maisha yao, ikiwa
ni njia sahihi ya kutafuta faraja ya kweli na uzima wa milele.
Hata hivyo, Lulu hakueleza kwa undani kile alichokiita kuchoka na
sarakasi za kidunia huku muda wote wakati anazungumza na mwandishi wetu
akilitaja jina la Yesu.
“Kwa hiyo, mimi na mama yangu kwa sasa tumejiweka mbali na ulimwengu,
kwanza niache niendelee na maombi,” alisema Lulu huku akifumba macho
kwa hisia kali.
Kwa upande wake mama Lulu aligoma kuzungumza chochote kuhusiana na suala hilo.

Note: Only a member of this blog may post a comment.