MKUTANO wa Chama Cha Wananchi (CUF) uliopangwa kufanyika leo katika ofisi za chama hicho Dar umeahirishwa ghafla.
Mwenyekiti wa chama hicho, Prof. Ibrahim Lipumba ilikuwa azungumze na wanahabari asubuhi ya leo jijini Dar, lakini mkutano huo umesitishwa ghafla hadi itakapotangazwa siku nyingine tena.
Waandishi wa habari wamejaribu kumuuliza Naibu Katibu Mkuu wa CUF Bara, Magdalena Sakaya kuhusu kile alichotaka kukizungumza mwenyekiti wao, Prof. Lipumba lakini Sakaya amewajibu kuwa wao hawajui kitu alichotaka kuwaambia wananchi.
Sakaya amesema kuwa, sababu kubwa ya kusitishwa mkutano huo ni wazee wa CUF kutaka kujua kwanza ni kitu gani mwenyekiti huyo anataka kuongea.
Wananchi nje ya ofisi za CUF wameshangilia wakiimba kwa kusema ‘Si mnaona, muziki wa Lipumba kuuzima hamuwezi’
Mmoja wa wananchi wanaoshangilia amesema wamefurahia kwakuwa wanaamini Mwenyekiti wao Lipumba hajiuzulu na yuko pamoja na wananchi.
Wananchi mbalimbali wanaoshangilia wanasema wanamuamini Lipumba na dalili iliyopo ni kuwa hawezi kujiuzulu maana anawasikiliza na ataendelea kuwa Mwenyekiti wa CUF.
Wapambe na mashabiki wa chama hicho leo walikua wamejazana nje ya ofisi kuu za chama hicho, wakiimba nyimbo za kumsifu Lipumba ambaye baadhi ya vyombo vya habari leo vimeripoti kwamba Prof Lipumba ametofautiana na maamuzi ya Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Shariff Hamad juu ya ushiriki wa Chama hicho katika UKAWA.
CHANZO: EATV

Note: Only a member of this blog may post a comment.