Ofisa wa NEC, Adam Nyando (kushoto) akimkabidhi fomu ya urais, Hashim Rungwe.
Ofisa wa NEC, Crecencia Mayalla (kushoto), akimpatia maelekezo mgombea namna ya kujisajili katika daftari la wagombea.
Hashim Rungwe (kushoto) akiwa na mgombea mwenza, Isa Abbas Husein (kulia), wakati wakipewa maelekezo ndani ya ofisi hizo.
1.Mgombea
urais, Hashim Rungwe kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma)
akiwaonyesha wanahabari (hawapo pichani) mkoba ulio na fomu ya kugombea
urais.
Hashim
Rungwe (kulia) akiwa na mgombea mwenza, Isa Abbas Husein (kushoto),
wakitoka ndani ya ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Wanahabari wakiwa nje ya ofisi za NEC wakimsubiri mgombea urais wa Chaumma.
Gari la Chaumma likiwa nje ya ofisi za NEC.
CHAMA cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kupitia mgombea wake, Hashim
Rungwe Spunda pamoja na mgombea mwenza, Issa Abbas Husein hii leo
wamechukua fomu ya kupeperusha nafasi ya Urais kupitia chama chao.
Mgombea huyo amechukua fomu hiyo mapema hii leo katika makao makuu
ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dar es Salaam, ambapo aliambatana
na mgombea mwenza kupitia chama hicho kwa ajili ya kuchukua fomu.
Aidha katika maelekezo ya fomu hiyo inamtaka mgombea kuzunguka mikoa
yote ya Tanzania na Zanzibar kusaka wadhamini 200 na hivyo kufikia
Agosti 21 fomu hiyo kurudishwa katika ofisi za tume.
(NA DENIS MTIMA/GPL)
Note: Only a member of this blog may post a comment.