Friday, August 21, 2015

Anonymous

MAGURI: Kuna Kigogo SIMBA SC Alitaka Kunitapeli

ELIAS MAGURII
Nicodemus Jonas, Dar es Salaam
STRAIKA ambaye ametupiwa virago Simba, Elius Maguri, amefunguka kuwa hakutaka kuondoka klabuni hapo lakini aliamua kuchukua uamuzi huo baada ya kiongozi mmoja wa Simba kutaka kumfanyia utapeli wa shilingi milioni tano.

Kuhusu tukio hilo, Maguri amezungumza na gazeti hili na kufunguka kama ifuatavyo:
“Kweli uongozi wa Simba ulinipa ruhusa ya kutafuta timu ya kuichezea kwa mkopo, timu nyingi zilinitafuta baada ya kupata taarifa hiyo na mojawapo tulikubaliana kila kitu na hata maslahi yake yalikuwa mazuri.

“Nikaiambia hiyo klabu iwasiliane na Simba, lakini ajabu ni kwamba kuna bosi mmoja akaiambia hiyo timu niliyozungumza nayo lazima itoe shilingi milioni tano. Lilikuwa jambo la kustajaabisha, wakahoji kuwa mimi nauzwa au natolewa kwa mkopo! Hapo ndipo dili likafa wakati hayo hayakuwa makubaliano yetu.

“IIiniuma sana, ikizingatiwa zilikuwa zimebaki siku mbili kabla ya dirisha kufungwa, ndipo nikaamua kuonana na viongozi nikaomba niwe huru.”

Upande wa Simba kupitia msemaji wao, Haji Manara, alipoulizwa juu ya taarifa hizo, alisema: “Tumeachana naye kwa matakwa ya mwalimu, huo mpango wa mkopo haukuwepo.”

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.