Dustan Shekidele, Morogoro
SHANGWE! Katika tukio linalotokea kwa nadra, wazee kumi ambao wameishi kinyumba kwa miaka mingi,Jumamosi iliyopita walibariki ndoa zao katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Monica, lililopo Tungi mkoani Morogoro, huku zoezi hilo likitikisa kila kona ya mjini hapa.
“Naomba Vigango vingine hapa Morogoro na Tanzania kwa ujumla kuiga mfano wa Mt. Clara, ambao waliamua kuwapa semina na kukubali kufunga ndoa,” alisema.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kigango hicho, Gilbert Robert alisema wao kama viongozi, wajibu wao ni kuwaelekeza waumini kuishi maisha ya kumpendeza Mungu, kwani kabla ya kufanikisha zoezi hilo, walifanya sensa na kugundua uwepo wa familia 44 zinazoishi bila ndoa, lakini ni kumi tu kati yao ndiyo walikubali kubariki.
“Baadhi waligoma wakidai hawana fedha za kufanya sherehe, hivyo sisi Kigango tumeamua kuwafanyia sherehe kwenye ukumbi huu wa masista,” alisema mwenyekiti huyo.
Wakati wa sherehe hizo ukumbini, wanandoa hao, wapambe, ndugu na jamaa waliburudika kwa chakula aina ya pilau na soda, huku kukiwa na vituko vya hapa na pale ikiwa ni pamoja na mabusu ya kizee kutawala.
Baada ya sherehe hiyo, wakati wa kurejea makwao tulishuhudia baadhi yao wakitembea kwa miguu huku akina mama wakizikunja shera zao, ingawa pia baadhi yao waliondoka kwa bodaboda, tena wakiwa wamepakizana kwa staili maarufu ya mishikaki.

Note: Only a member of this blog may post a comment.