MKUU
 wa wilaya ya Wanging’ombe, Frederick Mwakalebela ameibuka kidedea 
katika kura za maoni za kutafuta kuteuliwa kugombea ubunge jimbo la 
Iringa Mjini kwa kuwabwaga vibaya washindani wenzake 12.
Mmoja
 wa wagombea aliyebwaga katika kura hizo ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa
 Iringa, Jesca Msambatavangu (aliyekuwa mpambe wa Lowassa) alikuwa 
akipewa nafasi kubwa ya kuwa mshindi kwa kuzingatia nafasi aliyonayo 
ndani ya chama na nguvu yake kisiasa mjini Iringa.
Katika
 kura hizo, Mwakalebela alipata kura 4,388 huku Msambatavangu 
akijinyakulia kura 2,077 zilizompa ushindi wa pili, huku nafasi ya tatu 
ikienda kwa Dk Yahaya Msigwa aliyepata kura 1,097.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, Katibu wa CCM Manispaa ya Iringa, Elisha Mwampashi aliwataja wengine na kura zao kwenye mabano kuwa ni Dk Augustino Maiga (745), Mahamudu Madenge (423), Addo Mwasongwe (259), Nuru Hepautwa (191), Frank Kibiki (183), Michael Mlowe (183), Fales Kibasa (171), Aidan Kiponda (135), Peter Mwanilwa (79) na Agustino Mwilonge (66).
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, Katibu wa CCM Manispaa ya Iringa, Elisha Mwampashi aliwataja wengine na kura zao kwenye mabano kuwa ni Dk Augustino Maiga (745), Mahamudu Madenge (423), Addo Mwasongwe (259), Nuru Hepautwa (191), Frank Kibiki (183), Michael Mlowe (183), Fales Kibasa (171), Aidan Kiponda (135), Peter Mwanilwa (79) na Agustino Mwilonge (66).
Jimbo la Isimani
Waziri
 wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ametetea nafasi 
yake baada ya kuzoa kura 10,799 kati ya kura 12,560 zilizopigwa.
Lukuvi alifuatiwa kwa mbali na Mkuu wa Wilaya ya Misenyi, Festo Kiswaga aliyejipatia kura 1,237.
Katibu
 wa CCM Iringa Vijijini, Dodo Sambu aliwataja wengine na kura zao kwenye
 mabano kuwa ni Hamis Malinga (323), Sebastian Kiyoyo (155), , Elias 
Luputiko (62). 
Jimbo la Kalenga
Jimbo la Kalenga
Matumaini
 ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro kuwatumikia wananchi wa jimbo 
la Kalenga kwa kupitia nafasi ya ubunge huenda yakawa yamepotea kabisa 
baada ya kuambulia kura 674 kati ya kura 22,253 zilizopigwa.
Hii
 ni mara ya pili kwa Kandoro kuonesha nia ya kuwatumikia wananchi wa 
jimbo hilo bila mafanikio, mara ya kwanza ikiwa ni katika kura za maoni 
za 2010  alipoambulia kura 2,353 dhidi ya kura 2,819 alizopata aliyekuwa
 mbunge wa jimbo hilo, Dk William Mgimwa.
Katibu wa CCM Iringa Vijijini Dodo Sambu alimtaja mshindi wa kura hizo za maoni kuwa ni mbunge wa jimbo hilo anayemaliza muda wake, Godfrey Mgimwa aliyezoa kura 15,550.
Katibu wa CCM Iringa Vijijini Dodo Sambu alimtaja mshindi wa kura hizo za maoni kuwa ni mbunge wa jimbo hilo anayemaliza muda wake, Godfrey Mgimwa aliyezoa kura 15,550.
Wengine na kura zao kwenye mabano ni Jackson Kiswaga (3,439), George Mlawa (301) na Kibasa Kibasa (289). 
Jimbo la Mafinga Mjini
Jimbo la Mafinga Mjini
Afisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Cosato Chumi ameibuka mshindi kwa kuzoa kura 3,683.
Chumi
 amaye ushindi wake ulidhihiri kujionesha mara tu baada ya kutangaza nia
 ya kuwani ubunge katika jimbo hilo hivikaribuni, alifuatiwa kwa mbali 
na Zuberi Ngullo aliyepata kura 700 huku James Mgimwa akipata kura 378, 
Benjamin Balali kura 302 na Paulo Muyinga akiambulia kura 19. 
Jimbo la Mufindi Kaskazini na Mufindi Kusini
Jimbo la Mufindi Kaskazini na Mufindi Kusini
Hadi
 tunakwenda mitambo zoezi la kuhesabu kura lilikuwa likiendelea huku 
taarifa za awali zikionesha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, 
Mahamudu Mgimwa kuibuka mshindi katika jimbo lake la Mufindi Kaskazini.
Huko Mufindi Kusini, taarifa za awali zinaonesha kumpa ushindi mbunge anayemaliza muda wake, Mendrad Kigola. 
Jimbo la Kilolo
Jimbo la Kilolo
Hadi
 tunakwenda mitambani hakukuwepo na taarifa rasmi za matokeo ya jimbo 
hilo japokuwa wapambe wa wagombea wawili kati ya 15 waliojitokeza 
kuwania jimbo hilo, wamejitapa kushinda kura hizo za maoni.
Wakati
 wapambe wa mbunge anayemaliza muda wake, Profesa Peter Msolla wakidai 
kupata ushindi wa kishindo wa kura zaidi ya 13,000 nao wapambe wa Mkuu 
wa Wilaya ya Kaliua Tabora, Venance Mwamoto wanadai mgombea wao 
ameshinda japokuwa hawakutaja idadi ya kura walizopata.

Note: Only a member of this blog may post a comment.