Neno
‘Impersonator’ ni neno linalotosha kumtisha msanii yeyote. Unaposikia
kuwa kuna mtu anatumia jina lako kupata vya bure inaweza ikawa ‘Police
Case!’ Lakini, je unafahamu kuwa
Diamond alishawahi kujifanya Z-Anto akapendwa na mrembo fulani aliyedhani yeye ni Z-Anto?
Diamond alishawahi kujifanya Z-Anto akapendwa na mrembo fulani aliyedhani yeye ni Z-Anto?
Kabla
Diamond hajakuwa Platnumz, kabla hajapata umaarufu alionao sasa, Z-Anto
ndiye aliyekuwa akitikisa ‘airwaves’ na ngoma kama ‘Mpenzi Jini’ pamoja
na hit iliyomvukisha mipaka, ‘Binti Kiziwi.’ Wakati huo wasanii wengi
Afrika Mashariki walivuma sana kwenye Radio kabla hata kufikiria kutoa
Video. Nyimbo za Z-Anto zilitamba lakini wachache sana walijua sura yake
ikoje.
Hii ndiyo ilimpatia Diamond ‘opportunity’ ya kujifanya Z-Anto na kula vya bwerere kutoka kwa waliodhania yeye ni Z-Anto. Akiongea katika Heka Heka za kipindi cha ‘Leo Tena’ kwenye Clouds FM, Diamond alifichua kuwa, “Unajua mara ya kwanza niliogopa….lakini baada ya kuona kila mtu niliyekutana naye ananiamini halafu kulingana na nakula vitu kiubwete nikajifanya Z-Anto.”

Swali
ni je, alikuja kugunduliwa na kuchukuliwa hatua yeyote? Au je, Z-Anto
aliipata hii habari? Hauhitaji kujiuliza ilikuaje, ingia kwenye channel
yetu ya Mseto East Africa hapa upate uhondo kamili utakaokuchekesha na
kukushangaza sana

Note: Only a member of this blog may post a comment.