KIPIGO! Licha ya kujulikana na kuogopeka kwa ukorofi na ubabe
uliopitiliza, muigizaji wa filamu za Kibongo, Jimmy Mafufu, amechezea
kichapo kutoka kwa mkewe wa ndoa, Salma Mafufu kwa kile kilichoelezwa
kuchelewa kurudi nyumbani.
‘Akiteta’
na mwandishi wetu hivi karibuni, mmoja wa marafiki wa karibu na Mafufu,
ambaye anaishi mtaa mmoja na wanandoa hao, alisema tukio hilo la
fedheha lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita majira ya saa 3 usiku na
kuzua ‘mtiti’ mkali.
“Mafufu amepangiwa na mkewe kurudi nyumbani mwisho saa moja sasa siku
hiyo alinipigia simu na kuniomba niende nyumbani kwake, nilipofika
nikamkuta akigugumia maumivu kwenye mkono wa kushoto na kudai kuwa
alipigwa kwa kitu kizito na mkewe baada ya kuchelewa kurudi,” alisema
‘yuda’ huyo wa Mafufu.
Baada ya kupata umbea huo, mwandishi wetu alimtafuta Mafufu ambapo
alisema ni kweli alipigwa na mkewe na alipata mshtuko kidogo kwenye
mkono kwani alipigwa na kipande cha mti ila ugomvi ndani ya ndoa ni kitu
cha kawaida.

Note: Only a member of this blog may post a comment.