Hayo yamesemwa na katibu mkuu wa CCM wilaya Shinyanga mjini Bw.Charles Sangulo wakati akitangaza rasmi matokeo ya kura za maoni jimboni humo na kudai kuwa mchakato huo ulikuwa mkali uliojaa kashkash nyingi na vuta nikuvute za hapa na pale lakini palipo na ushindani lazima apatikane mshindi huku Mh.Steven Masele akiibuka mshindi na kuendelea kutetea jimbo la Shinyanga mjini.
Nao baadhi ya wananchi wa jimbo la Shinyanga mjimi hawakusita kutoa maoni yao kuhusiana na mchakato mzima katika kura za maoni na mabo yalikua kama ifuatavyo.
Aidha baadhi ya wagombea wengine walioshindwa kupata nafasi katika kinyanganyiro hicho wamelazimika kukubaliana na matokeo hayo kwa shingo upande huku wakidai kuwa malalamiko yao juu ya rushwa iliyokuwa imetawala katika kinyang'anyiro hicho yamekwama kwa madai kuwa yamekosa ushahidi wa kutosha hali iliyosababisha kubadilika kwa hali halisi ya matokeo hayo.
Na kwa upande wake msimamizi wa uchaguzi kura za maoni CCM kata ya Shinyanga mjini amemtangaza rasmi Bw.Gulam Hafiz Mukadama kuwa mshindi wa kiti cha udiwani kwa kupata kura 182 dhidi ya mgombea mwengine katika kinyang'anyiro hicho.

Note: Only a member of this blog may post a comment.