Polisi na kikosi cha uokoaji wakiwa kazini kwenye oparesheni ya jana.
Mtuhumiwa namba mbili wa mashambulizi ya Paris, Hasna Ait Boulahacen “The Cow Girl’.
Hasna Ait Boulahacen alivyopishana na askari kwenye lango la nyumba waliyokuwa wakiishambulia askari kuwasaka watuhumiwa.
Uvamizi wa askari katika Kitongoji cha Saint Denis, jana.
Polisi walivyojipanga kukivamia Kitongoji cha Saint Denis, Paris jana.
Watu walivyouawa kwenye shambulio la Ijumaa, Paris, Ufaransa.
Paris, Ufaransa
MWENDESHA mashtaka
nchini Ufaransa amethibitisha kwamba, mtuhumiwa namba aliyepanga
mashambulizi ya Paris, Abdelhamid Abaaoud ameuawa kwenye operesheni
maalum ya kumsaka ilioyoanza jana.
Abaaoud ndiye alikuwa akisakwa na polisi
waliovamia nyumba moja katika Kitongoji cha Saint Denis kilichopo
Kaskazini mwa Paris, Ufaransa.
Awali, mwendesha mashtaka wa Paris
Francois Molins alikuwa amesema Abaaoud na mshukiwa mwingine Salah
Abdeslam hawakuwa miongoni mwa watu wanane waliokamatwa.
Hata hivyo, miili ya watu wawili waliouawa ilikuwa bado haijatambuliwa na baada ya uchunguzi imebainika kwamba Abooud aliuawa.
Hayo yakijiri, wabunge nchini Ufaransa wanatarajiwa kupiga kura kuongeza muda wa kutekelezwa kwa hali ya hatari.
Wapiganaji wa Islamic State (IS), ambao
wanadhibiti maeneo ya Syria na Iraq walisema ndio waliohusika katika
mashambulio hayo yaliyoua watu 129 na wengine 400 kujeruhiwa Ijumaa
iliyopita.
Note: Only a member of this blog may post a comment.