Thursday, August 27, 2015

Anonymous

KUMEKUCHA! BAVICHA Waushambulia Msimamo wa CCM Kuwabana Wapinzani

IMG_0339
Mwenyekiti wa Bavicha Taifa, Patrobas Katambi akijadili jambo na Katibu Bavicha Taifa, Julius Mwita.
IMG_0335
Katibu Bavicha Taifa, Julius Mwita akiongea na wanahabari (hawapo pichani).
VIONGOZI wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha) Bavicha wamesema mwenendo unaofanywa na serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) dhidi ya wapinzani si wa haki, hivyo hawatauvumilika kamwe.

Viongozi hao ni Patrobas Katambi, Mwenyekiti wa Bavicha Taifa na Julius Mwita Katibu Bavicha Taifa walisema matukio mengi sana yamekuwa yakitokea dhidi ya wapinzani na chanzo cha ni CCM, kitu ambacho wanasema kuwa hawatakivumilia kiendelee.

Wakitoa mfano, viongozi hao wamesema katika majimbo ya uchaguzi wamejitangazia kuwa wameshinda bila kipingamizi kitu ambacho si cha kweli.

Majimbo wanayosema kuwa wameshinda tayari yameishakatiwa rufaa na ziko Tume ya Taifa ya Uchaguzi lakini CCM wanaendelea kusema kuwa wameshinda bila kikwazo.
Vilevile walipinga vikali hatua ya serikali ya kuwapiga marufuku wapinzani kutumia helikopta katika kampeni zao, jambo ambalo linaonyesha wazi kuzibana siasa za upinzani.

“Uchaguzi huu si wa CCM wala si wa Polisi bali ni wa Watanzania wote, hivyo ni lazima haki ifuate mkondo wake kwa kila idara iliyopewa mamlaka ya kusimamia suala fulani,” alisema Mwita.
Waliongeza kusema kuwa kama serikali haitasimamia haki wanao uwezo wa kuhamasisha vijana nchi nzima na kitakachotokea asilaumiwe mtu, alisema kiongozi huyo.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.