Kwa mujibu wa habari nyeti nilizotonywa sasa hivi kuna kizazaa cha fedha za kampeni zinazowafanya Lowassa, Chadema na UKAWA kwa ujumla kuwa katika mtafuruku mkubwa na mpaka sasa uliopelekea kuchelewa kuanza uzinduzi wa kampeni ya Urais wa ukawa.
Kizungumkuti kinaendelea wakati marafiki matajiri waliokuwa wanampa fedha azitakazo Lowassa wameona mambo yanakuwa magumu na badala ya fedha wameanza kumpa ahadi za kesho, kesho, kesho huku wakitazama upepo unapovuma.
Kuna habari nyingine kuwa kuanzia jana kuna ng'ombe zaidi ya 3,000 wanapakiwa wapelekwe sokoni kutoka kwenye ranchi moja kubwa sana iliyopo huko Handeni, sijuwi nayo inahusiana na Lowassa?
Kwa mujibu wa mtonyaji wangu anasema, Ndesamburo nae kagoma kutowa fedha, anasema Lowassa aliahidi atatowa fedha zote za kampeni yake yeye mwenyewe kwa hiyo asiulizwe yeye.
Mzee Mtei yupo mbioni kuwasiliana na Lowassa, Lowassa hapatikani kwa muda mrefu kwenye simu
Jamii Forums-Written By FaizaFoxy


Note: Only a member of this blog may post a comment.