Watanzania tulitegemea kuwa huu muungano Ungekuwa smart na taratibu zinazoeleweka zaidi kuliko za Chama kimoja kimoja. Matokeo yake yako Wazi kabisa, Chadema walikuwa na nguvu na uthubutu mwingi zaidi kabla ya kujiunga na ukawa.
Sasa hivi kipyenga cha kampeni kimezindiluliwa lakini ukawa hasa Chadema ni kama wako usingizini.
Chadema wanategemea zaidi drama za Lowassa kuliko mikakati yao walioyoipanga toka 2010.
Siioni ile Chadema iliyozunguka Kanda zote za Tanzania kutoa semina na warsha mbalimbali kuhusu taratibu,sera na mikakati ya Chadema.
Siioni Chadema ya kitaifa yenye uchungu na Tanzania, yenye kuwapigania watanzania maskini waliochoshwa na ufisadi.
Sasa hivi ni kama liwalo na liwe, na viongozi walioko makao makuu ni kama wapo pale kutimiza taratibu tu sio kupigania na kutetea chama.
Kama inafikia hatua majimbo matano au sita Ukawa wanakosa wagombea sababu ya uzembe na kuruhusu CCM kupita bila upinzani dhabiti hilo ni tatizo kubwa, Chadema ni chama kikubwa chenye Mizizi ya dhati kwenye ngome zake.
Hapo ndio ninapoona waziwazi pengo la Dr Slaa kwa jicho la tatu , kwamba Dr. Ndio alikuwa kiongozi anaesimamia na kuratibu shughuli za Chama kwa uthubutu zaidi.
Acha tuendelee kupiga kampeni kwa sanaa za Lowassa, maana movie zake zinavutia sana kuliko mikakati halisi ya chama.
Wakati huohuo tukisubiria hotuba za Mbowe zenye maneno matamu bila mikakati.!

Note: Only a member of this blog may post a comment.