Tuesday, August 11, 2015

Anonymous

Soudy Brown kwenye U Heard, leo ni Nuh Mziwanda na Idris… Kisa Shilole? (Audio)

photo-collage (1)
Kulikuwa na voice note ambayo ilichukua headlines sana, zinasikika sauti za watu wawili ambao ni Wema Sepetu na Nuh Mziwanda, kinachoongelewa ni ishu ya mapenzi. 

Baada ya hapo kukawa na ukimya pande zote mbili, Nuh aliandika kwenye ukurasa wake @Instagram kulalamika ishu ya sauti hiyo kusambazwa mitandaoni, kaongea na Soudy Brown na anasema ishu ya kuvuja na kusambaa mitandaoni kwa sauti hiyo kumefanya wawe na mgogoro na mpenzi wake, Shilole. 

Kuna tuhuma pia Nuh katoa kwamba wapo wanaume ambao wanaagizwa ili kumtaka kimapenzi mpenzi wake, Shilole.. mmoja wa waliotajwa kuhusika kumtafuta Shilole ni Idris Sultan, Soudy akamtafuta ili kusikia kuna nini kinaendelea. 

Idris kasema hakuna kitu cha aina hiyo, Shilole ni kama dada yake na wanapendana kama ndugu !!
Sauti ya U Heard hii hapa, Soudy Brown pamoja na Nuh Mziwanda pamoja na Idris.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.