Wednesday, August 19, 2015

Anonymous

Hatimaye ZARI The Bosslady Afunguka na Kutema CHECHE Kuhusu Sakata la Mtoto TIFFAH!

Hatimaye Zari The Bosslady ameamua kumjibu ex wake Ivan na swahiba wake King Lawrenc ambao wamekuwa wakimtupia madongo kuwa mtoto wake Tiffah si wa Diamond, ni wao.
King Lawrence alienda mbali zaidi kwa kutumia kampuni ya wanasheria kumtaka achukue vipimo vya DNA vya kichanga hicho chenye zaidi ya followers 80k kwenye Instagram.
Zari ametumia Instagram kuwajibu kwa kudai kuwa wanachofanya wawili hao ni visasi ambavyo anaamini hufanywa na vilaza!
“Visasi hufanywa na vilaza,” ameandika Zari kwenye Instagram.
“BO$$LADY anafahamu kuwa huzuni aliyonayo mtu mwenye chuki wakati akiangalia furaha na mafanikio yake ni adhabu tosha. Inabidi niyageuzie mgongo mambo yate ya kijinga yanayoendelea. Naendelea kuwaua kwasababu watu hutaka kuzima taa inayowaka zaidi kwao,” ameongeza.
Diamond tayari alishatoa majibu yake kufuatia hatua hiyo ya Ivan na Lawrence!
KAMA ULIMISS! BOFYA HAPA!

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.