Mke wa msanii wa muziki, H.Baba, Flora Mvungi amesema anajipanga
kuongeza watoto wawili wengine ili atimize malengo yake wa kuwa na
watoto wanne.
Flora ameiambia Bongo5 kuwa Mungu akimjalia atazaa watoto wengine wawili kwa haraka ili kutimiza malengo yake.
“Nawapenda sana watoto wangu wawili (Tanzanite na Africa) napumzika
kidogo halafu nataka nitafute wawili wa fasta,” amesema. “Mpango wangu
ni kuwa na watoto wanne, kwahiyo tumuombe Mungu alisimamie hili
litimie,” ameongeza.
Muigizaji huyo amesema mtoto wake Tanzanite anaonesha kila dalili ya kuja kuwa mwanamuziki mzuri.
“Tanzanite interest yake kubwa ni muziki, sema sasa hivi ndio ana
miaka miwili na tunataka kumkazia kwanza asome ndio tumwingize kwenye
muziki.”
-Bongo5

Note: Only a member of this blog may post a comment.