Director Adam Juma amejibu lawama ambazo amekuwa akizipata kwa muda
mrefu kuhusu video zake kutochezwa na vituo vya kimataifa kama MTV na
Trace licha ya kuwa na ubora mkubwa.
Adam amesema kuwa sababu kubwa ya video nyingi anazofanya kushindwa kuchezwa zinaanzia kwa wasanii wenyewe.
Hiki ndicho amekisema kupitia 255 ya XXL ya Clouds Fm:
“Mi mtaendelea kunilaumu mpaka mtafika sehemu mtakuja kugundua,
hata akija kufanya mtu mwingine mwisho wa siku hamuwezi mka solve,
lazima mjue source ya matatizo…mnaweza mkafikiri labda mimi sitaki hizo
video ziende huko, lakini swala sio hilo video zisiende huko, wasanii
wenyewe pia sio wavumilivu…Alikiba kafanya video akaja akaitoa,
kachelewa sana kuitoa, Trace wanatumia wiki tatu kui review
video…hawakubali kupiga video baada ya watu wengine kupiga wanataka wao
waanze kupiga wao, kwahiyo kuna wasanii wengine wajanja, wanaipeleka
kule video miezi miwili mitatu mpaka ije kupita wakishapewa hiyo
exclusive baada ya siku mbili tatu ndio wanaaachia bongo…Sasa mtu
anataka ashut leo leo ipigwe Tanzania halafu iende ikapigwe na
Trace…sasa mtu mwingine anakua ananilalamikia mimi bila sababu utafikiri
mimi nafanya kazi bure tu. “– AJ

Note: Only a member of this blog may post a comment.