AY amedai kuwa wasanii wengi wa Tanzania wanashindwa kufanikiwa
kimataifa kutokana na kukosa na network yaani kufahamiana na watu vya
kutosha.
“Unajua network na kujuana na watu mbalimbali ndio inayoweza
kumsaidia msanii kupiga hatua katika kazi yake na kufanya vizuri katika
muziki,” AY ameiambia E-News ya EATV.
“Wasanii wengi bila kuwa chini ya uongozi hawawezi kufanya chochote
ndio maana mimi nikaamua kujitolewa kuwasimamia wale ambao naamini
wanaweza kufika mbali wakiwa chini ya usimamizi.

Note: Only a member of this blog may post a comment.