Thursday, August 6, 2015

Anonymous

FUMANIZI LA AIBU GUEST MOROGORO! Mke Azimia Baada ya Kumshuhudia Mumewe LIVE!

Mwanamke mmoja aliyetajwa kwa jina la Salome amejikuta akipoteza fahamu baada ya kumfumania mumewe akiwa na mwanamke mwingine ndani ya gesti moja maarufu iliyopo maeneo ya Msamvu, Morogoro.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, walisimulia kuwa awali walimuona mwanamke huyo akiwa amekaa upande wa baa kwenye gesti hiyo huku akiwa amejitanda upande mmoja wa kitenge kama vile alijificha asionekane na watu.

“Baadaye aliinuka haraka na kwenda upande wa vyumba vya kulala wageni ndiyo mara tukasikia purukushani halafu kuna mwanamke akatoka mbio bila viatu, sasa tulipoenda ndani kujua nini kilichotokea tukamuona yule mama akiwa sakafuni na mwanaume ambaye baadaye tulimjua kuwa ni mumewe akiwa anahangaika kumuamsha.

“Inawezekana kabisa alipata mshtuko kutokana na ule mchepuko wa mumewe, kwa sababu kuna taarifa kuwa ni binamu yake huyu mama,” kilisema chanzo chetu.

Hata hivyo, baadhi ya wasamaria wema walimsaidia mume wa Salome, kumpepea mkewe huku wakimlaumu kwa kuchepuka hovyo kiasi cha kuhatarisha maisha ya ‘wife’ wake ambaye baadaye alizinduka na kuondoka eneo la tukio.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.