MWANAMKE
aliyefahamika kwa jina la Amina Kamagi Kuzwa (60) mkazi wa
Nzega, Tabora, anadaiwa kujinyonga kwa kile kilichosemekana ni kwa
sababu ya kuugua kwa muda mrefu.
Akizungumza na Amani, mtoto wa marehemu, Elizabeth Mayunga alisema mama yake alikuwa akiugua kwa muda mrefu bila wao kujua ugonjwa uliokuwa ukimsumbua mpaka pale alipomchukua na kuja naye Ndege Beach jijini Dar kwa ajili ya matibabu.
“Mwezi wa tano mwaka huu tulipata msiba hapa Dar, ikatubidi tuusafirishe kwenda kuzika Nzega. Kumbe kipindi hicho mama alikuwa akiumwa. Nilishangaa sana kwani kipindi cha nyuma alikuwa na hali nzuri tu. Nilipomuuliza alisema anasumbuliwa na vidonda vya tumbo.
“Nikaamua kuja naye huku. Juni 23, mwaka huu nikampeleka Hospitali ya Mwananyamala akiwa analalamika tumbo linamuuma na kujaa gesi. Nikampeleka Hospitali ya Masista, Tegeta akagundulika ana vidonda vya tumbo na fangasi,” alisema Elizabeth.
“Tulirudi nyumbani, nikampa dawa anywe. Hali yake ikawa inaridhisha, tukalala. Kumbe saa 12 asubuhi aliamka kwenda kujisaidia ndiyo akaenda kujinyonga kwenye mti wa mwarobaini kwa kutumia mtandio wake,” alisema mtoto huyo.
“Nilipata taarifa kutoka kwa mwanangu ambaye aliamka muda huo kwa lengo la kwenda kujisaidia lakini alikaa nje ya mlango wa choo akijua bibi yake yumo msalani. Ikabidi aingie na alipotoka ndipo akaanza kumtafuta kwa kuzunguka nyumba na kumkuta akining’inia mtini. Naamini mama aliamua kuchukua uamuzi huo kwa vile aliugua kwa muda mrefu,” alisema Elizabeth.
Mwili wa marehemu Amina ulisafirishwa wiki iliyopita kupelekwa katika Kijiji cha Negeleo, wilayani Handeni, Tanga kwa mazishi yaliyofanyika Jumapili iliyopita. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina.

Note: Only a member of this blog may post a comment.