Friday, August 28, 2015

Anonymous

Beki SIMBA SC Aondolewa Kikosini Uturuki, Kuikosa Nigeria!

Banda1
Beki na kiungo mkabaji wa Simba, Abdi Banda.
Saleh Ally, Kartepe
BEKI na kiungo mkabaji wa Simba, Abdi Banda, ameondolewa katika kikosi cha Taifa Stars kitakachoivaa Nigeria katika mechi itakayopigwa jijini Dar es Salaam, Septemba 9.


Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa, amethibitisha hilo na kusema ni kutokana na maumivu ya nyama.
“Anatakiwa akae hadi wiki tatu, maana yake hawezi tena kuivaa Nigeria na sasa mazoezini tumeshamuondoa, badala yake atakuwa akija kuangalia kama unavyomuona,” alisema Mkwasa.


Kuhusiana na hilo, Daktari wa Taifa Stars, Michael Yomba amesema Banda ameumia nyama ambazo ni lazima kupumzika.
“Kihesabu mapumziko hutakiwa kuanzia siku kumi hadi 21. Kwa yeye, ningeshauri apumzike hadi hizo siku 21 hata baada ya kurejea Simba,” alisema Yomba.


Banda aliumia juzi wakati wakifanya mazoezi ya kukimbia kwa kasi ndani ya mita 100 na John Bocco, Simon Msuva na Rashid Mandawa ndiyo walionekana kuwa hatari kwa kasi.
Banda ambaye alijiunga na Simba akitokea Coastal Union, alikuwa kati ya waliokuwa wanafanya vizuri lakini baadaye aliumia na kutolewa nje.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.