Barnaba amewashauri wasanii wenzake kutoiharibu Bongo Flava kwa kutaka kufanya muziki kama wa Nigeria.
Akiongea na E-News ya EATV, Barnaba alisema, “Wasanii wengi
ukiwauliza wanakwambia wanaenda na wakati wanafanya muziki wa kibiashara
mimimi sikubaliani na hilo suala, mimi nadhani biashara ipo pale pale,
inategemea na uimbaji na unahama vipi,” amesema msanii huyo.
“Hautakiwi kuwa unahama unaimba muziki wa kukimbia kwakuwa watu
wengine wamehama, unaweza ukajikuta unabugi, unatakiwa utwist kidogo
namna ya uimbaji. Mfano kama Christian Bella, hajahama kwenye muziki
wake wa bendi lakini ameitwist kidogo, muziki wake ni ule ule wa bendi
lakini badala ya dakiki nane, sasa hivi wake una dakika 3 au 4,
amechanganya kidogo na Bongo Flava.”
“Nawashauri wasanii wenzangu kusikiliza sana muziki tofauti tofauti
hata miziki yetu ya zamani ambayo ilikuwa bora hadi leo. Unaweza
ukachukua hata nyimbo hizo lakini ukaziboresha zaidi ukapata muziki
mzuri. Ule muziki wa Nigeria wao wenyewe wanachukua asilimia nyingi huku
kwetu lazima tuwe wabunifu wa muziki wetu.”

Note: Only a member of this blog may post a comment.