WAZUNGU wa Simba, Dylan Kerr na 
Dusan Momcilovic, wamekuwa kivutio kikubwa kwenye mazoezi ya timu hiyo 
iliyopiga kambi huku Tanga kutokana na wao wenyewe kufanya mazoezi zaidi
 ya hata makocha wengine kwenye Ligi Kuu Bara.
Makocha hao kwa nyakati tofauti wamekuwa wakifanya mazoezi ambapo awali Momcilovic ambaye ni raia wa Serbia, hivi karibuni alizunguka uwanja wanaofanyia mazoezi Simba wa Chuo cha Sekomu uliopo Magamba, mara kumi na kunyoosha viungo huku akimalizia na mazoezi ya jumla na wachezaji wake ambapo alitumia takriban nusu saa kukamilisha kila kitu. Kuona hivyo, Kerr akatamani kumlipa ambapo baada ya kumalizika kwa mazoezi ya wikiendi iliyopita na ya juzi Jumatatu, kocha huyo alikacha kwa muda kupanda basi la timu hiyo na kuamua kukimbia kwa umbali wa zaidi ya Kilomita Mbili.
Awali, alivyofanya hivyo kila mmoja alishindwa kufahamu nia ya kocha huyo lakini walikuja kupata jibu walipomkuta njiani akikimbia na alipoliona basi hilo akalisimamisha na kupanda huku akionekana kuwa yupo fiti.
Championi limekuwa likiwashuhudia makocha hao wakifanya hivyo ambapo ni tofauti na makocha wengi waliopo hapa Bongo.
“Nimekuwa nikifanya hivi ili kuuweka fiti mwili wangu kwani nachukia sana kuwa na kitambi na nikiwa kama kocha wa viungo napaswa kuwa fiti ili niimudu vilivyo kazi yangu,” alisema Momcilovic ambaye ana mwili mkubwa wenye afya.


Note: Only a member of this blog may post a comment.