Wednesday, July 15, 2015

Anonymous

NGOMA Aomba Msaada wa MWASHIUYA Yanga!

1 (1)Mshambuliaji mpya wa Yanga, Mzimbabwe, Donald Ngoma.
Wilbert Molandi, Dar es Salaam
MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga, Mzimbabwe, Donald Ngoma, amesema mabao mengi anayoyafunga yeye ni kwa kutumia mguu, lakini safari hii akiwa na timu hiyo anataka kufunga kwa vichwa huku akiwataka mawinga na mabeki wake kumpigia krosi safi. 

Mawinga wa timu hiyo ni Simon Msuva, Geofrey Mwashiuya, Deus Kaseke, Andrey Coutinho na mabeki wa pembeni ni Oscar Joshua, Mbuyu Twite, Juma Abdul na Haji Mwinyi.

Mzibambwe huyo, alijiunga na Yanga akitokea Platinum FC iliyokuwa inashiriki Ligi Kuu ya Zimbabwe akisaini mkataba wa miaka miwili.
IMG-20150630-WA0065 
Geofrey Mwashiuya
Mshambuliaji huyo, tangu atue kuichezea Yanga, amecheza mechi mbili za kirafiki na zote alifunga bao moja moja dhidi ya KMKM alilofunga kwa kichwa na lingine na Kombaini ya Majeshi alilomchambua kipa.

Akizungumza na Championi Jumatano, Ngoma alisema yeye siyo mzuri wa kufunga mabao ya vichwa ila ni mkali kwa kupiga mashuti na kumchambua kipa ndani na nje ya 18.

Ngoma alisema, akiwa na Platinum alifanikiwa kufunga mabao 16 kati ya hayo 10 kwenye ligi kuu na mengine kwenye mashindano mbalimbali, kati ya hayo ni machache ambayo alifunga kwa kichwa, hivyo amepanga akiwa na Yanga kufunga kwa njia hiyo.

Aliongeza kuwa, ili afanikishe malengo yake ya kufunga mabao kwa njia ya kichwa, basi amewataka mawinga wa timu hiyo kuhakikisha wanampigia mipira mizuri ya krosi na kona kuhakikisha anafanikisha ndoto zake kwa kuanzia kwenye ligi kuu na michuano mingine.

“Mimi siyo mzuri wa kufunga mabao ya kichwa licha ya kufunga pale inapotokea mpira unapokuja katika mazingira mazuri ya kufunga ninapokuwa uwanjani.
“Usione nimefunga bao kwa njia ya kichwa katika mechi ya kwanza dhidi ya KMKM, ukaona ni mzuri, hapana, mimi ni mzuri wa kufunga kwa kumchambua kipa au kupiga mashuti ndani na nje ya 18.

“Lakini safari hii nikiwa na Yanga, nimepanga kufunga idadi kubwa ya mabao kwa njia ya kichwa, ninaamini hilo nitafanikiwa kama mawinga watanichezesha vizuri kwa kunipigia krosi nzuri,” alisema Ngoma, mwenye umbile kubwa.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.