Mashaka kisusi NDANI ya Mwezi
Mtukufu wa Ramadhani, mama mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara
moja, mkazi wa maeneo ya stendi, wilayani Misungwi mkoani Mwanza
anadaiwa kuchezea kichapo kutoka kwa mumewe baada ya kumfumania akiwa na
kimada, Risasi Jumamosi linatiririka.
Akivuja damu baada ya kuminyiwa kichapo.
Tukio hilo lililowaacha watu midomo wazi lilijiri mwanzoni mwa wiki
hii ambapo kwa mujibu wa mashuhuda, awali mwanamke huyo alipita maeneo
hayo akiwa anaongea na mtu kupitia simu yake ya mkononi, lakini baada ya
muda alirudi akiwa analia huku damu chapachapa. “Alitonywa kwa njia ya simu kwamba mumewe yuko kilabuni na kimada, ndipo alipomuibukia lakini nasikia mumewe kakolea kwa huyo kimada, hivyo akamgeuzia kibao kwa kumtaka aondoke. Alipogoma sasa ndiyo akalazimika kumpa kichapo hevi hadi kumtoa damu,” alisema shuhuda huyo.
Akizidi kupewa kichapo na mumewe.
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, baada ya kichapo hicho,
mwanamke huyo alitimkia kwenye stendi hiyo ambapo wasamaria wema walimpa
msaada baada ya kumuona anavuja damu usoni lakini alipoulizwa kulikoni,
alikataa kuzungumzia fumanizi hilo kwa undani na kutaka arudishwe kwa
mumewe akalipe kisasi.“Nirudisheni! Nirudisheni! Nasema nirudisheni kule nikalipe kisasi, sikubali,” alisikika akisema mwanamke huyo huku akiangua kilio.

Note: Only a member of this blog may post a comment.