Saturday, July 11, 2015

Anonymous

MUNGU MKUBWA, HATIMAYE BANZA ATOKA HOSPITALI!


Gladness mallya BAADA ya mwanamuziki wa Dansi nchini, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’ kulazwa katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar kwa siku saba, hatimaye ameruhusiwa kurejea nyumbani baada ya kupata nafuu.

Mwanamuziki wa Dansi nchini, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone.
Banza aliruhusiwa kutoka hospitalini hapo, Jumatano iliyopita ambapo kwa mujibu wa kaka yake ana nafuu japokuwa bado hali si shwari kwani daktari aliyekuwa anamtibu aliwaeleza kwamba ndugu yao huyo ana tatizo la upungufu wa damu.
“Tunamshukuru Mungu mgonjwa wetu ameruhusiwa japo bado hali yake haijatengamaa kwani tofauti na matatizo ya awali ya fangasi za kichwani, anakabiliwa na upungufu wa damu hivyo tumeshauriwa tumpe vyakula vya kuongeza damu,” alisema Hamis.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.