Kuna
baadhi ya nchi duniani uvutaji wa sigara ni kitu cha kawaida na
ukiangalia nchi kama Jamaica wamekuwa wamehalalisha wazi matumizi ya
bangi ambayo watu wake wamekuwa wakiitumia hadharani bila tatizo.
Lakini
kwa upande wa china matumizi jayo yamepigwa marufuku na sasa Serikali ya
nchi hiyo imetangaza wazi kuanzia leo Juni 1, ukikutwa unavuta sigara
hadharani katika ameneo ya wazi au eneo la karibu na shule ama hospitali
unalipa faini.
Awali
China ilipitisha sheria hiyo lakini haikuisimamia kama ambavyo
imetangaza kwa sasa na sehemu zitakazokuwa zikiangaliwa zaidi ni mji
mkuu wa nchi hiyo Beijing.
Ripoti
ilionyesha takribani watu milioni 300 wanatumia sigara na sasa kutakuwa
na faini ambapo ukikutwa unavuta hadharani utatozwa fedha ya kichina
10,000 ambayo ni sawa na dola 1600.
Wauzaji wa sigara wametakiwa kuuza bidhaa hiyo kuanzia umbali wa mita 100 kutoka maeneo ambayo yamekatazwa.

Note: Only a member of this blog may post a comment.