Nicodemus Jonas, Dar es Salaam
MABINGWA wa kihistoria wa Kombe la Kagame, Simba SC, wametajwa kuwa chanzo cha Yanga kutumia karibu Sh milioni 200 mpaka sasa katika usajili wa wachezaji sita waliothibitisha kuichezea timu hiyo msimu ujao.
Yanga kama wanavyojiita wa kimataifa, wameendelea kuonyesha jeuri ya hela baada ya kuwazidi kete Simba katika vita ya kuwania saini ya fowadi wa Mgambo, Malimi Busungu ambaye alikuwa kwenye rada za Simba kwa muda mrefu.
Akizungumza na Championi Jumatatu, mmoja wa viongozi wa Kamati ya Usajili ya Yanga, amefunguka kuwa wamelazimika kuingia gharama kubwa kusainisha wachezaji kutokana na Simba kupenda kuingilia rada zao pindi wanapojua ofa za Yanga.
Aliongeza kuwa, kuna wachezaji waliosajiliwa kipindi hiki kwa kitita kirefu kwa presha ya Simba ambao wamekuwa wakitoa ofa ya upinzani, jambo ambalo limewalazimu kupandisha ofa kwa mchezaji. Championi linafahamu kuwa Yanga walilazimika kuongeza dau la Sh milioni tano katika kitita cha Sh milioni 30 cha Deus Kaseke baada ya nyota huyo kupewa ofa nono zaidi na Simba muda mfupi kabla ya kumwaga wino Yanga, ikidaiwa alitakiwa kwa milioni 42 na mazaga mengine.
“Tumeona ni bora tufanye usajili wa chinichini kuhusu dau la mchezaji. Kila tukimtaka mchezaji fulani, lazima wenzetu Simba waingilie, nao utasikia wanamtaka. Jambo hili limesababisha wachezaji kujiweka katika dau kubwa, hivyo hutulazimu kutumia gharama kubwa zaidi ya kile tulichopanga awali.
“Ndiyo maana tumepanga kutotaja ofa zetu kwa wachezaji ambao hatujamalizana na hii ni kutokana na mchezo unaochezwa na Simba, ambao wanasuburia mchezaji fulani anatakiwa kwa kiasi hiki na wao wanajitokeza,” alisema mjumbe mmoja wa kamati ya usajili Yanga.
Zaidi ya Sh milioni 200 mpaka sasa zimemwagwa na Yanga katika kunasa saini za wachezaji Haruna Niyonzima (mil 70) na Mbuyu Twite (mil 30) waliokuwa wamemaliza mikataba huku Kaseke akinaswa kutoka Mbeya City kwa mil 35, Busungu (Mgambo, mil 25) na kipa Benedict Tinoco (Kagera Sugar, mil 10) kujumlisha na mishahara yao.
Wachezaji wengine wanaotajwa kuweza kuanguka saini muda wowote ni fowadi Mzimbabwe, Donald Ngoma na kiungo Mcameroon, Youssef Sabo ambao dau lao kwa ujumla ni zaidi ya Sh mil 90.

Note: Only a member of this blog may post a comment.