Monday, March 7, 2016

Anonymous

UTI: Ugonjwa Linalosumbua Wanawake Wengi-2

UrinaryTractInfection.jpg URINARY_TRACT_INFECTION
Wapo wanawake ambao wamekuwa wakidhani kwamba tatizo la kutokwa na uchafu ukeni ni ugonjwa wa UTI (Urinary Tract Infection), wazo hilo si sawa kwani huo ni ugonjwa tofauti kabisa na UTI.
Tunapozungumzia maambukizi katika njia ya mkojo yaani UTI, inamaanisha ni kutoka eneo la nje ya utupu hadi kwenye kibofu na kutoka kwenye kibofu hadi kwenye figo. Kama maambukizi yako katika eneo la kutoka kwenye kibofu hadi kwenye figo, kitaalam huitwa Lower Urinary Tract Infection na yakihusisha eneo la juu ya kibofu jina hubadilika na kuitwa, Upper Urinary Tract Infection.

Maambukizi katika njia ya mkojo au kama unavyojulikana kwa wengi UTI huathiri mfumo wa mkojo ikiwa ni pamoja na Ureter ambayo ni kama bomba linalosafirisha mkojo kutoka kwenye figo, pia kibofu cha mkojo na mrija wa kutolea mkojo nje yaani Urethra.

Ugonjwa huu unaathiri zaidi kibofu cha mkojo na Urethra lakini unaweza pia kuathiri figo. Maambukizi haya yakiathiri sehemu za chini za kibofu cha mkojo kitaalam huitwa Simple Cystitis au Bladder Infection na maambukizi hayo yakitokea sehemu za juu za mfumo wa mkojo huitwa Pylonephritis au Kidney Infection.

Ugonjwa huu husababishwa na bakteria anayeitwa Escherichia Coli (E. Coli) na tatizo hili husababishwa kwa kiasi kikubwa na bakteria ambao makazi yao ya kawaida ni kwenye utumbo mpana na hivyo huwa wanapatikana pia kwenye haja kubwa.

Lakini baadhi ya watu wanaweza kupata tatizo hili kutokana na kuingiwa na fangasi ingawa pia zipo sababu nyingine chache. Bakteria wa Escherichia Coli hawasababishi peke yao UTI bali huambatana na wengine waitwao Staphylococcus, Saprophyti cus, Pseudom Onas, Enterobacter na kadhalika. Maambukizi katika njia ya mkojo lazima yawe ni kwenye njia ya mkojo na si pengine popote.

SABABU ZA UTI KWA WANAWAKE
Mara nyingi maambukizi haya kwa wanawake husababishwa na kutojisafisha vizuri sehemu za siri na kuvaa nguo za ndani zilizochafu. Pia huweza kusababishwa na matumizi ya pedi za kike zenye kemikali ya kukata harufu ambazo huua bakteria wa asili wa eneo la uke na kuwapa fursa bakteria wanaosababisha maradhi kuzaliana kwa wingi.

Halikadhalika upungufu wa homoni ya wanawake iitwayo Oestrogen husababisha bakteria wanaosababisha maambukizi katika njia ya mkojo kuzaliana kirahisi. Matumizi ya baadhi ya dawa kwa muda mrefu, unywaji wa vinywaji vyenye sukari kwa muda mrefu na kutokunywa maji ya kutosha pia huchangia tatizo hili.

Uwepo wa mawe katika figo na mirija ya figo pia ni mojawapo ya chanzo cha maambukizi haya katika njia ya mkojo.
Sababu nyingine inayosababisha UTI ni matumizi ya maji machafu wakati wa kujisafisha au kuoga.
Itaendelea wiki ijayo.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.